Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uganda, Sam Kutesa.
Uwezekano wa Waziri wa Mashauri
ya Kigeni wa Uganda, Sam Kutesa, kushinda cheo cha Urais wa Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa kumeanzisha mjadala mkali nchini Uganda, huku
wakereketwa wa haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda wakipinga
asichaguliwe.
Ingawa Urais huo katika Umoja wa Mataifa hauna
mamlaka makubwa lakini wakereketwa hao wanasema kuwa cheo hicho cha
heshima hakipaswi kupewa Afisa wa cheo cha juu katika Serikali ya Uganda
kwa sababu Taifa hilo la Afrika Mashariki lilipitisha sheria ambayo
wanasema inawabagua wapenzi wa jinsia moja.Maelfu ya wakereketwa hao wametia sahihi katika ombi kwenye mtandao wakisema kuwa kuchaguliwa kwa Bwana Kutesa kama Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ni madharau kwa maadisi ya Umoja wa Mataifa.
Seneta wa New York, Kirsten Gillibrand pia itakuwa "hatua ya kusikitisha kumwona Waziri wa Mashauri ya Kigeni kutoka taifa lililopitisha sheria isiyo na haki, ya kudhulumu na ya kubagua kuwa kinara wa shirika hilo la kimataifa.."
Hapa alikuwa akigusia Sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja iliyopitishwa Februari ambayo inaruhusu watu wanaoshiriki mapenzi hayo kufungwa maisha gerezani.
Bwana Kusesa, mwanadiplomasia mkongwe mwenye umri wa miaka 65 alisema hivi majuzi kuwa "waafrika wengi wanachukia ushoga."
Urais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hauna mamlaka na hutolewa kwa mtu kutoka maeneo mbalimbali kila mwaka.
Mwaka huu ni zamu ya Afrika kumteua Rais huyo na Bwana Kutesa amekubaliwa na Bara lote bila kupingwa.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment