
Habari
za kusikitisha zilizotufikia hivi punde zinaarifu kuwa Mwigizaji
maarufu na mkongwe katika fani ya vichekesho nchini Tanzania, Said
Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small (59) amefariki dunia baada ya
kuugua kwa muda mrefu.
Mzee Small amefikwa na umauti majira ya saa 4 za usiku wa Juni 7, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhumbili.
Akiongea kwa njia ya simu mke wa marehemu, Bi Fatuma Saidi, ameithibitishia , kuwa Msanii Said Ngamba hatunae.
Bi
Said amesema kuwa marehemu mumewe amefikwa na umauti baada ya hali yake
kubadilika jana (Juni 7) asubuhi na kumbikiza Muhimbili ambako
alishinda nae akipatiwa matibabu na majira ya saa tatu usiku alirudi
nyumbani na kumwacha kijana wake akimwangalia mgonjwa na ilipotimu saa
tano usiku kijano huyo alirudi na kusema baba amefariki.
“Nikweli Mzee Small amefariki”….yalikuwa ni maneno machache yaliyobenba uchungu mzito kufuatia kifo cha mumewe.
Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Tabata Mawenzi, Dar es Salaam.
Blog ya bongomail.blogspot.com inatoa pole kwa familia yake yote, Ndugu jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo.
MAISHA NA SANAA
Katika
historia fupi, Mzee Small alipata elimu ya msingi katika Shule ya
Mingumbi huko Kilwa mkoani Pwani. Mbali na kuwa mkongwe, Mzee Small kila
ulipobahatika kuzungumza naye alikuwa na kawaida ya kutamba kuwa yeye
ndiye msanii wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha runingani.
Mzee
Small alianza sanaa hiyo yapata miaka 31 iliyopita na alipata
kufundishwa na mwigizaji Said Seif ‘Unono’ (ambaye pia kwa sasa ni
marehemu).
Mbali
na kushiriki sanaa katika vikundi mbalimbali, Mzee Small wakati wa uhai
wake ametumika katika vikundi vya mashirika kama vile Reli, NASACO na
mengine mengi, ambayo kwa sasa hayajihusishi tena na shughuli hizo.
Mzee
Small alianza kujulikana sana katika fani ya uchekeshaji hasa pale
alipoibuka na mchezo uliojulikana kama 50, 50, 100, na ule wa Mjini
Shule uliomwelezea mwanamke wa kijijini aliyeolewa mjini.
Mbali
na kutamba na michezo hiyo, Mzee Small alikuwa ni mcheshi na mwenye
kupenda utani wakati wote, aliibuka na kichekesho kisemacho Nani Mwenye
Haki, ambacho baadaye alikiboresha zaidi.
Baadaye
aliibuka na kitu kingine kikali kilichokwenda kwa jina la Nani Kama
Shule, huku akiwa amewashirikisha wakali wengine kama King Majuto,
Kingwendu na wachekeshaji wengine wanaotamba kwa sasa Bongo.
Mzee
Small alikuwa ndiye mmiliki wa kundi la sanaa linalojulikana kama
Afro-Dance ambalo alilisajili mwaka 1994 kwenye Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) na kutoa ajira kwa vijana wa mitaani.
Pamoja
na kuwa na uzoefu wa kisanaa, lakini mkongwe huyo hakuwahi kuwa na
mpango wa kujiunga na kundi lingine, ila alichokuwa akifanya ni kurekodi
na wasanii wengine alipokuwa akiitwa kwa makubaliano maalum.
Pia
mkali huyo wa vichekesho enzi za uzima wake na uhai wake alikuwa
akijishikiza katika duka moja Kariakoo la Home Shopping Centre
kimatangazo.
Kutokana
na vichekesho, Mzee Small huwa anatania kuwa sanaa ilimpa mke wa ndoa
katika televisheni ambaye ni Bi Chau huku akianisha kuwa mkewe, Bi
Fatuma huwa hana tatizo lolote na Bi Chau kwani anajua kinachoendelea
kuwa ni kazi tu.
Mzee
Small amefariki na kuacha mjane na watoto watano, watatu wa kiume na
wawili wa kike. Kipindi cha uhai wake Marehemu Small alikuwa akisisitiza
sana elimu na Sanaa iwe baada ya kumaliza masomo yao.
MATESO YA KIAFYA
Wakati
akiendelea na harakati za kisanaa, mwaka juzi Mzee Small aliripotiwa
kupatwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alipokuwa kwenye shughuli za
kisanaa Kanda Ziwa.
Ugonjwa huo ulimpa mateso makubwa huku akiwa hana msaada wowote.
Wakati
akiteseka na kiharusi alipata tatizo linguine kwenye ubongo huku
akitakiwa kila mwezi kwenda kliniki kwa ajili ya ‘check-.
Hakika
kila nafsi itaonja mauti na leo Mzee Small ambaye mbali na kuiburudisha
alikuwa akitoa mafunzo kwa jamii yetu kupitia kazi zake, leo ameonja
mauti na Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema ampunzishe Mkali huyo wa
vichekesho mahali pema.
Habari hizi za kusikitisha zimeripotiwa na chanzo cha kuaminika ambacho
kimeeleza kuwa alizidiwa na ugonjwa wa presha uliopelekea kifo chake.
Muigizaji huyo amekuwa akisumbuliwa na magonjwa kwa muda mrefu hali iliyompelekea kulemaa viungo hususani mkono wake.
Taarifa hizi ni mwiba mwingine kwa tasnia ya filamu nchini ikiwa ni wiki
moja imepita tangu marehemu George Tyson afariki kwa ajali ya gari.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment