Leo jioni, mjini Iringa kwenye viwanja vya Mwembetogwa, Mh Mwigulu
Nchemba alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, alisema kuwa Watanzania
wana uhuru mkubwa sana wa kuongea mpaka wanakosa adabu hata kwa wazee
wao "..najua mnaona natumia lugha kali, lakini ndio kawaida yangu kusema
ukweli, ...natamani niwe Rais wa nchi hii ili niwafundishe adabu
Watanzania, ndio!" Labda inawezekana alimaanisha kuwafundisha adabu
Watanzania fulani, lakini kwakuwa alikuwa akiongea kwa jazba aliteleza
ulimi, au alimaanisha hivyo. Watu waliohudhuria mkutano huo walipigwa na
butwaa, aliliona hilo na kubadilisha mada haraka. Aliwafurahisha watu
pale aliposema"..kule kwetu Singida, ng'ombe mpole ndie anaekamuliws
sana maziwa, lakini yule mkorofi anaachwa, kadhalika (serikali)
inawatoza kodi wajasiriamali wadogo bila msamaha lakini wawekezaji
wakubwa wanasamehewa mabilioni ya fedha!) suala hilo ameahidi kupambana
nalo.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali zenye mantiki na mashiko.
0 comments:
Post a Comment