Serikali ya nigeria imebatilisha
amri yake ya awali ya kupiga marufuku maandamano ya kutaka wasichana
waliotekwa nyara Nigeria kuachiliwa.
Wasichana hao zaidi ya miambili walitekwa nyara
na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram katika eneo la Chibok Kaskazini
mwa Nigeria.Hata hivyo wanaharakati hao wapewa onyo kujizuia na ghasia wakati wa maandamano hayo.
Afisa mkuu wa polisi amesema kuwa maandamano hayo ambayo yamekuwa takifanywa karibu kila siku ni tisho kwa usalama wa nchi na kwamba kuna hofu kuwa wapiganaji wa kiisilamu huenda wakapenya na kuingia kwenye maandamano hayo.
Kauli mbiu ya maandamano hayo ni ''Bring Back Our Girls'' yaani turejesheeni watoto wetu, na waandamanaji wanasema kuwa maandamano yao yamekuwa ya amani.
Kundi la kiisilamu la Boko Haram, limesema kuwa liko tayari kuwaachilia wasichana hao ikiwa serikali nayo itawaachilia wapiganaji wake wanaozuiliwa.
0 comments:
Post a Comment