Facebook

Thursday, 19 June 2014

Rooney katika mgogoro mzito Brazil

Wayne Rooney achezeshwe katika nafasi gani ?
Njama dhidi ya Wayne Rooney yaweza kuhatarisha matarajio yao katika kombe la dunia. Frank Lampard ameonya.
Uchunguzi wa nafasi yake Rooney katika timu hiyo ulizidi wakati Rooney alipocheza katika nafasi ambayo hakufaa, Uingereza iliposhindwa mabao 2-1 na Italia.
“Shughuli hizi nyingi kwa mchezaji mmoja hazitamsaidia yeyote,”alisema Lampard, mwenye umri wa miaka 35.
Raheem Sterling, aliyecheza katika nafasi ya kawaida ya Rooney, alisema kuwa kurudi kwao katika nafasi zao za kawaida kwaweza kuiletea uingereza mafanikio wakati timu hiyo itakapokutana na Uruguay siku ya Alhamisi.
Hata hivyo, Sterling, mwenye umri wa miaka 19 alisema kuwa itakua uamuzi wa mkufunzi wao kufanya hivo.
Alizidi kusema kuwa nafasi aliyoicheza Rooney katika mchuano uliopita, ndiyo iliyokua nafasi yake, naye Rooney akapewa nafasi hiyo, hivyo hakuweza kuitumia kikamilifu.
Kocha Hogson alaumiwa kwa kumchezesha Rooney asikofaa
Sterling alifanya utani kwa kusema kuwa alitarajia hatamwona mchezaji mwenza katika timu ya Liverpool, Luis Suarez uwanjani Arena de Sao Paulo wakati wa mechi yao.
Hata hivyo alisisitiza kuwa Uruguay ilikua na wachezaji wengine mashuhuri, zaidi na Suarez anayeuguza jeraha.
Mchezo mzuri ulioonyeshwa na Sterling katika mechi dhidi ya Italia umefanya ionekane kuwa Rooney aweza tena kunyimwa nafasi ya katikati ambayo ana mazoea nayo.
Lampard aliongeza kusema kuwa ni tukio la kutatanisha haswa katika mtazamo wa timu na tukio hilo laweza kugeuka na kuwa njama badala ya kuwa la kujadiliwa.
Lampard ambaye hakupata kupewa nafasi ya kucheza katika mechi yao ya kwanza alizidi kusema kuwa mchezaji mmoja akianza kulengwa mara kwa mara, timu nzima itaadhirika.
Rooney alifunga mabao 17 akiichezea Manchester United musimu uliopita lakini hajaifungia nchi yake bao lolote katika 9 ya michuano ya kombe la dunia ambayo ameshiriki.
Wayene Rooney achezeshwe katika nafasi gani ?
Mchezaji wa zamani wa Uingereza Allan Shearer, alisema heri Rooney aondolewe kikosini ikiwa hatapata kutumiwa katika nafasi ambayo aliizoea.
Hii ni licha ya pasi yake iliyoletea Daniel Sturridge kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Italia.
Uamuzi wake Mkufunzi Roy Hodgson unakuja kabla ya mchuano muhimu kwani wakipoteza dhidi ya Uruguay, wataondolewa wakiwa katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958.
Lampard alizidi kusema kuwa angependa wachezaji wa Uingereza kulenga kupata matokeo mazuri badala ya kucheza vizuri kisha kushindwa kama ilivyokua katika mchuano wao na Italia.
Aliiwaambia kuwa bidii yao yote waiweke katika mchuano huo moja, iwe ni kama fainali ya kombe la dunia kwao, kwani ikiwa watashindwa, itamaanisha kuondolewa kwao katika kombe la dunia.
Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

Related Posts:

  • Mashabiki wa Ghana wazamia Brazil     Zaidi ya mashabiki mia mbili wa soka kutoka Ghana walioingia Brazil kwenda kutazama Kombe la Dunia wameomba hifadhi ya ukimbizi nchini humo.     Polisi wa Brazil katika mji wa Caxias do Sul wa… Read More
  • LIVERPOOL NA BARCA WAKUBALIANA JUU YA SUAREZ   Liverpool wamefikia makubaliano ya kumuuza Luis Suarez kwenda Barcelona. Ada ya uhamisho inadhaniwa kuwa takriban pauni milioni 75. Suarez alijiunga na Liverpool mwaka 2011 akitokea Ajax, kwa pauni milioni 22.7. A… Read More
  • Refa wa fainali za Kombe la Dunia atajwa....!              Nicola Rizzoli amechaguliwa na Fifa kuwa mwamuzi katika mchezo wa fainali - Kombe la Dunia Brazil 2014 kati ya Ujerumani na Argentina.  &n… Read More
  • David Rudisha azidi kung'ara Olimpiki.   David Rudisha ameshinda mbio za mita 800 wanaume katika mbio za Diamond League za Scotland. Mara ya mwisho kuwa nchini Uingereza Rudisha alishinda medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki ya London 2012. Mwa… Read More
  • Robben: ‘Argentina hawana lolote’ Winga  wa kidachi Arjen Robben amekiponda kikosi cha Argentina kwa kiwango duni walichokionesha mpaka sasa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia, na kusema kuwa hata ushindi wao walioupata dhidi y… Read More

0 comments:

Post a Comment