Facebook

Thursday, 19 June 2014

Tanzania kubadili sheria kuhusu Shisha

Uvitaji wa Shisha ni sawa na uvutaji wa sigara kulingana na madaktari
Waziri wa afya nchini Tanzania, amesema kuwa Tanzania inapanga kutathmini sheria ya sasa kuhusu matumizi ya Sisha ili kufanya mageuzi au kubadili sheria hiyo matumizi ya Shisha.
Dkt Seif Rashid Selemani amesema kuwa sheria hiyo italenga kulinda afya ya watanzania hasa walio na uraibu wa Shisha na pia kuhakikisha kuwa wanaotumia Shisha katika sehemu zengine duniani wanapata kubadili mfumo wa maisha ili kulinda afya zao.
Hii ni baada ya taarifa ya awali kuwa serikali ilikuwa tayari imechukua hatua kupiga marufu bidhaa hiyo ambayo inaenziwa sana hasa na vijana.
Uraibu huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye ladha tofauti tofauti ambayo hutiwa ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa mirija, umeshika kasi sana Tanzania hasa miongoni mwa vijana mjini Dar Es Salaam.
Baadhi ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya kiafya ikilinganishwa na uvutaji wa Sigara.
Lakini wataalamu wanaamini kuwa uvutaji wa Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta sigara miamoja.
Madaktari walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha wakisema kuwa waraibu wanakabiliwa na tisho la kuugua Saratani sawa na hatari inayowakabili wavutaji wa sigara.


Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment