Facebook

Thursday, 19 June 2014

Uholanzi yasonga mbele, Brazil

Uholanzi ni timu ya kwanza kufuzu kwa mkondo wa pili wa kombe la dunia.
Uholanzi ilitoka mabao 2-1, nyuma na kuishinda Australia mabao 3-2 katika mchuano wa kusisimua wa kombe la dunia huko Rio de Janeiro, siku ya Jumatano.
Oranje kama inavyojulikana timu ya Uholanzi, iliiadhibu kwa urahisi Uhispania mabao 5-1 katika mchuano wao wa kwanza, lakini walilazimishwa kujikaza katika mchuano huu wa pili ilikupata ushindi.
Arjen Robben aliweka Uholanzi kifua mbele katika dakika ya 20.
Dakika moja baadaye, Australia walisawazisha kupitia mchezaji Tim Cahill.
Cahill baadaye alionyesha upande wake mbaya wakati alipomtendea dhambi Bruno Martins na kumfanya kuondolewa uwanjani katika machela.
Cahill aliadhabiwa na hili lamaanisha hatakuwa katika mechi inayokuja ya Australia dhidi ya Uhispania.
Mile Jedinak aliifungia Australia bao la pili kupitia penalti katika dakika ya 58 baada ya Daryl Janmaat kuugusa mpira ndani ya eneo lao la lango.
Robin van Persie pia alionyeshwa kadi ya njano kwa kumtendea visivyo Matthew Spiranovic, naye hatakuwa katika mchuano baina ya Uholanzi na Chile.
Hata hivyo katika aliifungia uholanzi bao la kusawazisha kunako dakika ya 68.
Uholanzi ni timu ya kwanza kufuzu kwa mkondo wa pili wa kombe la dunia.
Kuendelea kwa Uholanzi katika raundi ya pili ya kombe la dunia, bado kutaamulia katika mchuano wa mwisho kwani tofauti ya mabao yaweza kutatanisha.
Uholanzi inahitaji kushinda mechi hiyo ilikuepuka kuchuana na wenyeji brazil katika mkondo wa pili .
Mlinzi wa upande wa kulia wa Australia, Ryan McGowan aliupiga mpira uliowapita walinzi wa Uholanzi na kumfikia Cahill aliyeupiga ukagonga kizingiti cha juu ya lango la Uholanzi na kuingia.
Hili laweza kuawa moja kati ya mabao bora kabisa katika michuano hii.
Martins, aliyechezewa visivyo na Cahill, alibadilishwa na mchezaji Memphis Depay, nao Uholanzi wakabadilisha mchezo wao na kuanza kutumia mtindo wa 4-3-3.
Muda mfupi baadaye, Australia walijipata nyuma wakati mkwaju wa yadi 30, wake Depay ulimponyoka kipa wa Australia, Ryan, na kuingia.
Mkwaju wake Nigel de Jong pia ulizuiwa Uholanzi ikitafuta bao la nne.
Australia ilikua na nafasi pia ila haikuweza kupata bao la kusawazisha na matumaini yao ya kufika mkondo wa maondoano yakawa yanadidimia.


Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

Related Posts:

  • Liverpool waanza vibaya mechi yao ya kwanza ya kirafiki. Liverpool Leo hii huko Brondby, Denmark walichapwa Bao 2-1 katika Mechi yao ya kwanza ya Ziara yao ya kabla Msimu mpya kuanza walipofungwa na Wenyeji wao Club Brondby IF.   Wakiwa chini ya Meneja wao Bren… Read More
  • OSCAR "SIJUI CHA KUSEMA" Kiungo mshambuliaji wa Brazil na Chelsea, amesema hajui nini kimewatokea baada ya mfululizo wa matokeo mabaya katika mashindano ya Kombe la Dunia huko nchini kwao. Hata hivyo, alikubali timu yao haikucheza vyema na … Read More
  • ADHABU YA POWELL YAPUNGUZWA    Bingwa wa zamani wa mbio za mita 100 Asafa Powell na Sherone Simpson wote kutoka Jamaica wamepunguziwa adhabu ya kufungiwa, kutoka miezi 18 hadi miezi sita. Uamuzi uliotolewa na mahakama ya usuluhisi wa m… Read More
  • Ujeruman yapokelewa kwa shangwe.   Maelfu ya mashabiki wa soka nchini Ujerumani wamejitokeza mjini Berlin kuwalaki wachezaji wa timu ya taifa walioshinda Kombe la Dunia. Sherehe kubwa zimefanyika katika eneo la Brandenburg Gate, ambapo wacheza… Read More
  • Adidas watarajia makubwa baada ya kuingia mkataba mnono na Manchester United   1.Klabu; Manchester United Kampuni; Adidas Thamani(mwaka); £75m Miaka 10; £750m 2.Klabu; Real Madrid Kampuni; Adidas Thamani(mwaka); £31m Miaka 8; £248m 3.Klabu; Chelsea Kampuni; Adidas Th… Read More

0 comments:

Post a Comment