Facebook

Thursday, 19 June 2014

Siagi ya Uruguay yanaswa Brazil

Siagi ya Uruguay ilinaswa na maafisa wa uwanja wa ndege Brazil
Wasimamizi wa uwanja wa ndege Brazil wamezuia takriban kilo 39 za siagi ya karameli kutoka timu ya mpira ya Uruguay walipowasili kwa michezo ya kombe la dunia.
Siagi hiyo ilikamatwa kutoka kwa timu hiyo ilipowasili katika uwanja wa ndege wa Confins karibu na kambi yao wanakofanyia mazoezi,Sete Lagoas.
Siagi hiyo inayojulikana kama ''dulce de leche'' inaumaarufu sana Uruguay lakini wasimamizi Brazil walisema kuwa kutengenezwa kwake kwa maziwa kunahitaji uhifadhi wa kiwango cha juu cha usafi ambao timu hiyo ya Uruguay haina uwezo wa kutimiza hilo.
Mashabiki wao tayari wameanza kulaumu utepetevu wa timu hiyo iliyocharazwa na Costa Rica mabao 3-1 kutokana na ukosefu wa siagi hiyo katika maankuli yao.

Msemaji kutoka kitengo cha kilimo cha Brazil aliiambia Reuters kuwa timu hiyo inaweza kurudishiwa siagi yao iwapo itapeana stakabadhi inayohitajika kuidhinisha kuingia nchini Brazil la sivyo watalazimika kusubiri hadi baada ya kukamilika kwa kampeini yao nchini humo .
Mlinda lango wa zamani wa timu hiyo Juan Castillo alisema kuwa timu hiyo ilibeba siagi hiyo walipoelekea Afrika Kusini mwaka wa 2010 na hawakuwa na tatizo lolote kutoka kwa wakuu nchini humo.
Dulce de leche inatengenezwa kwa maziwa,hamira na vanila na hutumiwa sana kwa kupakwa kwenye mkate,biskuti na kuchanganywa na matunda.

Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

0 comments:

Post a Comment