Facebook

Wednesday, 3 September 2014

Nigeria kuishitaki Schalke kwa FIFA

Shirikisho la soka Nigeria limesesema litaishitaki klabu ya Schalke ya Ujerumani kwa Fifa baada ya klabu hiyo kukataa kumruhusu mshambulizi Chinedu Obasi kushirki michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015.
Hata hivyo klabu ya Schalke imesema kuwa sababu ya kukosa kumruhusu mchezaji huyo kuondoka ni kwamba pasi yake ya usafiri iko katika ubalozi huku viza yake ikitayarishwa kabla ya kuanza kwa michunao ya klabu bingwa Ulaya.
Afisa wa habari wa Super Eagles Ben Alaiya amsema kwamba wana mechi mbili ambazo tayari zimeidhinishwa na Fifa.
"nchi yetu ina haki ya kukabidhiwa mchezaji wake Chinedu Obasi kwa michuano ya kufuzu kwa kombe hilo. ''
Nigeria ambao ni mabingwa wa Afrika, watamenyana na Congo mnamo tarehe sita Septemba. Siku nne baadaye watatoana kijasho na Afrika Kusini. Nigeria imekasirishwa na
Schalke kuhusu mchezaji wake Obasi.

Vilabu hushurutishwa kuwaruhusu wachezaji wa kigeni kuchezea nchi zao katika michunao ya kimataifa pindi wanapotakiwa na nchi zao kucheza.
Klabu hiyo ya Bundesliga inamtaka Obasi, kucheza dhidi ya Borussia Monchengladbach katika ligi hiyo na mechi itakayochezwa dhidi ya Chelsea katika michunao ya klabu bingwa Ulaya tarehe 13 na 17.
Alaiya aliongeza kusema kuwa mchezaji anapaswa kurejea kushirki majukumu ya kimataifa pindi anapohitajika.
"katibu wa timu amefanya awezalo na sasa tutachukua hatua kwa kushitaki Schalke kwa Fifa. ''
Wakati huohuo Nahodha wa Nigeria amejiondoa katika mechi mbili za kufuzu kwa michuano ya taifa bingwa Afrika.

Related Posts:

  • John Bocco aanza mazoezi Captain John Bocco ameanza mazoezi kidogo kidogo katika Gym ya kisasa ya Azam FC hapa Chamazi - Azam Complex, Captain anaendelea vizuri na jeraha lake alilolipata Kigali Rwanda akiitumikia timu yake ya Azam FC. Hii ni leo asb… Read More
  • Yanga kupinga maamuzi ya TFF juu ya Okwi.Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi kuwa huru. Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande… Read More
  • Danny Welbeck aing'arisha Uingereza.Danny Welbeck straika mpya wa Arsenal alifunga mara mbili kuisaidia England kuifunga Switzerland kwa bao 2-0 katika mchezo wa kufuzu michuano ya Euro 2016. Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United aliziona vyavu dakika ya… Read More
  • FAIDA YA MAN UTD 'KUTETEREKA'Manchester United imetangaza kuporomoka kwa faida ya kila mwaka wa fedha katika mwaka ambao David Moyes alikuwa meneja. Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England imesema kipato halisi kimeporomoka kwa asilimia 84 na kufikia takriban … Read More
  • Maicon aondolewa timu ya taifa ya Brazil kwa kashfa ya "Ushoga" Brazil ilicheza mechi ya kirafiki na Colombia kule Miami Florida, hapo jumamosi, ikaibuka na ushindi wa 1-0, kwa goli lililofungwa na mshambuliaji wa Neymar. Hivi sasa Brazil inajiandaa kukipiga na Ecuador hapo Jumatano, Se… Read More

0 comments:

Post a Comment