Kampuni ya Binslum Tyres Co. Ltd....chini ya Mkurugenzi wake, Nassor Binslum sasa imeingia mkataba wa miaka miwili wa shilingi 360 milioni na klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya.
Katika
mwaka wa kwanza, Mbeya City itapokea kiasi cha shilingi 180 milioni, na
mwaka wa pili itapokea kiasi kama hicho....watavaa jezi yenye nembo ya
RB ikiwa ni betri maarufu za kampuni hiyo.
Kampuni
ya Bin Slum Tyre Company Limited leo imeingia mkataba rasmi wa
kuidhamini timu ya soka ya Mbeya City Council ya jijini Mbeya katika
hafla fupi ya utiaji saini mkataba huo uliyofanyika katika ukumbi wa
ofisi za jiji la Mbeya.
Mkataba
huu utakuwa wa miaka miwili, ambao utawafanya Mbeya City kunufaika na
kiasi hicho cha fedha kwa muda huo wote wa mkataba.
Akiongea
wakati wa utiaji saini wa mkataba huo jijini Mbeya, Mkurugenzi wa ,
Binslum Tyre Mohamed Binslum, alisema “Tumefikia makubaliano haya baada
ya kuona uongozi wa timu ya Mbeya City umejipanga vizuri katika
kuendesha timu yao, na kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi wa
Jiji la Mbeya pamoja na mikoa ya Kanda ya Kusini, hivyo itakuwa ni fursa
nzuri kwa kuzitangaza betri zetu za RB ambazo pia Mbeya ni soko letu
kubwa”.” Kampuni yetu ina bidhaa nyingi kama vile aina nzuri ya matairi
ya Double Star na Vee Rubber”. Aliongeza Binslum
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora
zaidi.
0 comments:
Post a Comment