Facebook

Monday, 9 June 2014

Mwanamke ajitoa mhanga,ashambulia kambi Nigeria

Rais Goodluck Jonathan
Mwanamke aliyejitolea mhanga alijiripua nje ya kambi ya jeshi, kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
Wanajeshi wawili walijeruhiwa vibaya.
Afisa wa jeshi alisema kwamba mwanamke huyo aliyevaa hijabu, alikaribia kambi kwa piki-piki katika jimbo la Gombe.
Aliripua bomu wakati akihojiwa na wanajeshi.
Mwandishi mmoja katika eneo hilo, anasema siyo kawaida kwa mwanamke kushambulia kwa kujitolea mhanga nchini Nigeria, na jimbo la Gombe limekuwa salama kwa jumla.
Hakuna kundi lilodai kufanya shambulio hilo.
Lakini kundi la Waislamu la Boko Haram, limekuwa likilenga makambi ya jeshi na polisi.

Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com....

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment